Tuesday, March 27, 2012

DUKA JIPYA LA KIAFRIKA LAFUNGULIA NCHINI BELGIUM

Kutana na kijana mtanashati mwenye huduma bora kabisa dukani hapo.
Kwa waafrika wote mnaoishi nchini Belgium,sasa umefika wakati wa kuona kama bado mpo nyumbani kwa kupata mahitaji yenu ya chakula cha asili ya Afrika.

Njoo sasa ujipatie kila aina ya chakula toka kwetu barani Afrika Voeding Winkel Africaanse ndio jibu lako la mahitaji yote ya nyumbani.Kuna Dagaa,Unga wa Muhogo,Viazi ulaya,Bamia,Mihogo,Mafuta ya Mawese,Samaki watamu aina zote toka nyumbani Afrika,Mchele safi wa kunukia,soda aina zote toka Afrika,pilipili zetu zile za kuwasha,Nazi,Magimbi na mengineyo mengi sana ambayo ukija mwenye dukani utafaidi kile unachoambiwa.

Bado kuna Vitenge,Khanga na Bazee aina mbalimbali dukani hapo,Dvd`s za Kitanzania,Nigeria na Burundi zinapatikana dukani hapo.kwa kutaka kujua zaidi kabla hujafika dukani hapo unaweza kupiga simu namba .ukitaka kufika mwenyewe anuani ni hii Graaf De Broquevillestraat 1- Mol.Waafrika iwe wewe ni MBURUNDI,MTANZANIA,MGHANA,MNIGERIA,MSOMALI,MNYARWANDA,SENEGAL,GUINEA tuungane pamoja kujivunia kilicho chetu kwa kupeana habari juu ya duka hili.

Maharage ya kopo na ya kawaida,Viungo vya mapishi,maziwa ya Nido,mafuta ya mawese,unga wa chapati n.k
 Samaki aina zote na kuku toka Afrika,usisahau kisamvu(Sombe) ambacho ni kitamu kwa Ugali na Wali,kuna Dagaa toka pande za Kigoma Aisee usichelewe kufika Voeding Winkel mjini Mol kwa mambo matamu toka Afrika.
Hello.
Tangazo kwa kina Mama,Wasichana na Wanawake wote wa kiafrika wanaoishi nchini Belgium na Holland kuwa,Kuanzia sasa hawana haja ya kuumiza vichwa pale wanapotaka kutengenezwa nywele zao iwe kusukwa,kutengenezwa staili na kupambwa siku ya harusi.jibu ni Azashaplus Hair ambao watakutengeneza nywele zako vyema na kukufanya kila mmoja apende kukutazama kwa muonekana wako mzuri wa nywele.

Fanya kupiga simu ili kuweka appointmet ukatengeneze kichwa chako piga namba hii +32 492 253 601 au tuandikie kwa email Keishaone@ymail.com

Azashaplus kadhalika wanapamba kumbi za harusi,upigaji picha za video na picha za kawaida  kwa bei nafuu kabisaa.jitahidi kwenda na wakati kwa kuwasiliana nasi.kwa wakazi wa Belgium Azashaplus wanapatikana Mol na kwa wakazi wa Holland tupo Den Haag.ukiliona tangazo hili tafadhali usisite kumjulisha na mwenzako.ahsanteni sana              Keisha One.